# kama mmoja Hii inazungumzia kundi la watu ambalo lipo kama mtu mmoja. # Hakuna hata mmoja wetu atakayeenda hemani kwake ... hakuna hata mmoja wetu atakayerudi nyumbani kwake Sentensi hizi mbili zina maana moja na hapa zinaonesha msisitizo. "Tutakaa hapa wote" # Lakini sasa Maneno haya yanaonesha ni kitu gani watu walikuwa wanazungumza. # kama kura inavyotuongoza Hii inahusisha kuzungusha mawe madogo ili kujua Mungu anataka nini.