# Alipofika "Samsoni hakusafiri pekeyake, alikuwa akiongozwa na watu waliokuwa wamemfunga kwa kamba" # Lehi Hili ni jina la mji uliopo Yuda. # akaja juu yake kwa nguvu Roho wa Bwana alimchochea Samsoni. "akamfanya Samsoni kuwa na nguvu" # Kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitambaa cha kuteketezwa "Alizikata kamba zilizokuwa mikononi mwake kwa urahisi kama kitambaa kilichokuwa kinateketezwa" # Kitambaa Hiki kimetokana na mmea ambacho hutumika kutengenezea nyuzi na nguo.