# Yote unayoyafanya ni kunichukia! Hunipendi "Hunipendi mimi kabisa" # Kitendawili Huu ni mchezo ambao wachezaji wanatakiwa wagundue jibu kutokana na swali gumu. # Angalia hapa "angalia" inamanisha "sikiliza" "nisikilize mimi" au "kuwa makini kwa ninachotaka kukwambia" # kama sijawaambia baba yangu au mama yangu, nikuambie wewe? Samsoni anamkemea mke wake baada ya mkewe kumlazimisha amwambie jibu. # kwa siku saba ambazo sikukuu yao iliendelea Yaweza kuwa na maana ya 1)"katika siku saba za sikukuu yao" au 2) "katika siku saba zilizobaki za sikukuu yao" # Siku ya saba "siku ya 7" # Alimlazimisha sana "Aliendelea kumlazimisha ili amwambie"