# Samsoni akashuka Timna Neno "kushuka" linatumika kwa sababu Timna ipo juu ya ilipokuwa nyumba ya baba yake na Samsoni. Timna ni jina la mji uliopo kwenye bonde la Soreki. # Na, tazama, kuna simba mdogo wa alikuja "Tazama" ni neno lililotumika ili kumfanya msomaji awe makini kwa tukio linalofuata katika simulizi. # alikuwa akiunguruma "alikuwa akimtisha." Hii ni sauti ya simba ambayo huitoa akiwa anataka kuvamia kitu. # Roho wa Bwana ghafla akaja juu yake Roho wa Bwana akamchochea Samsoni. Akamfanya kuwa na nguvu sana. # Kumrarua ... vipande Akamrarua vipande viwili. # hakuwa na kitu mkononi mwake Hakuwa na kitu mkononi mwake ikimaanisha kuwa hakuwa na silaha yoyote.