# Samsoni akashuka kwenda Timna Neno "kushuka" linatumika kwa sababu Timna ipo juu ya ilipokuwa nyumba ya baba yake na Samsoni. Timna ni jina la mji uliopo kwenye bonde la Soreki. # mmojawapo wa binti za Wafilisti. "binti" ni njia moja wapo ya kuelezea kuwa mwanamke huyu alikuwa hajaolewa. # Sasa mkanichukulie awe mke wangu. Samsoni aliwaomba wazazi wake wazungumze na wazazi wa yule mwanamke kuhusu ndoa.