# Mtu wa Mungu Hii inamaanisha kuwa mtu huyu alitumwa na Mungu. # kuonekana kwake kulikuwa kama malaika wa Mungu, wa kutisha sana. "Nilimwogopa kwa sababu alionekama kama malaika wa Mungu" # Tazama "sikia" # Utazaa mtoto mwanaume "kuzaa mtoto wa kiume" au "kuwa na mtoto wa kiume" # chakula chochote ambacho sheria inasema kuwa si safi Kitu ambacho Bwana amesema hakifai kuliwa kinaonekana kuwa ni najisi. # Mnaziri wa Mungu. "alitolewa kwa Mungu kama Mnaziri" # tangu alipokuwa tumboni mwako mpaka siku ya kufa kwake Hii inasisitiza kuwa itakuwa hivi kwa kipindi chote cha maisha yake.