# Kuwaangamiza na kuwadhulumu Haya maneno mawili yana maana moja ya kusisitiza ni kwa namna gani wana wa Israeli walikuwa wanateseka. # Miaka kumi na nane "miaka 18" # waliokuwa ng'ambo ya Yordani Hii inamaanisha waliokuwa mashariki mwa mto Yordani. # iliyoko Gileadi "huu mji pia uliitwa Gileadi" # Yuda ... Benyamini "Yuda" na "Benyamini" inasimama badala ya watu waliotoka katika makabila haya. "watu wa kabila la Yuda ... watu wa kabila la Benyamini" # Nyumba ya Efraimu "nyumba" inasimama badala ya kabila la Efraimu. # Israeli akasumbuliwa sana "israeli" inasimama badala ya watu wa Israeli. "watu wa Israeli wakateseka sana"