# waliendelea kutenda maovu mbele za Bwana "waliendelea kufanya mambo ambayo Bwana alisema ni uovu" # mbele za Bwana "mbele za Bwana" inawakilisha kitu ambacho Bwana anakifikiria au kuwaza juu ya jambo fulani. # Maashtoreti Huu ni wingi wa Ashtoreti aliyekuwa anaabudiwa kama mungu wa uongo kwa namna mbalimbali. # Wakamsahau Bwana na hawakamsujudia tena "waliacha kabisa kumwabudu Bwana" # Wakamsahau Bwana Kumtii na kumwabudu Bwana inazungumzwa kama kitendo cha watu kumwacha Bwana na kwenda mahali pengine. # Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli Kitendo cha Bwana kuwa na hasira kinafananishwa na moto uwakao. # akawauza mikononi mwa Wafilisti na katika mikono ya wana wa Amoni Bwana akaruhusu Wafilisti na Waamoni wawashinde Waisraeli. # mkononi mwa "mkono" unawakilisha nguvu na utawala.