# Zebuli Hili ni jina la mwanaume. # aliposikia maneno ya Gaali, mwana wa Ebedi "maneno" inawakilisha kile alichokisema. # Gaali ... Ebedi Haya ni majina ya wanaume. # hasira yake ikawaka Kitendo cha kuwa na hasira kinafananishwa na moto unaoanza kuwaka. # ili wapate kudanganya Zebuli anamdanganya Gaali na watu wa Shekemu. # nao wanauchochea mji dhidi yako "wanawashawishi watu wa mji waasi dhidi yako" # mji "mji" inawakilisha watu wa mjini.