# Gaali ... Ebedi Haya ni majina ya wanaume. # Abimeleki ni nani, na Shekemu ni nani, hata tumtumikie? Gaali anatumia swali kusisitiza kuwa watu wa Shekemu hawawezi kumtumikia Abimeleki. # Abimeleki ni nani, na Shekemu ni nani, Maswali haya yanamaana moja. Gaali anamuelezea Abimeleki kama Shekemu maana mama yake na Abimeleki alitoka Shekemu. # Je, si mwana wa Yerubaali? Na Zebuli si afisa wake? Gaali anatumia swali kusisitiza kuwa watu wa Shekemu hawawezi kumtumikia Abimeleki. # Yerubaali Hili ni jina lingine la Gideoni. # Zebuli Hili ni jina la mwanaume. # Watumikieni watu wa Hamori, baba yake Shekemu Gaali anamaanisha watu wa Shekemu wawatumikie watu wa uzao wa Hamori. # Kwa nini tunapaswa kumtumikia? Gaali anatumia swali kusisitiza kuwa watu wa Shekemu hawawezi kumtumikia Abimeleki. # Laiti watu hawa wangekukuwa chini ya amri yangu "natamani ningekuwa nawatawala watu wa Shekemu"