# Ndugu za mama yake waliongea kwa niaba yake kwa viongozi Hii ina maana ya kwamba ndugu za mama yake Abimeleki walizungumza na viongozi, wakapendekeza wamfanye Abimeleki kuwa mfalme. # wakakubali kumfuata Abimeleki "wakakubali Abimeleki awe kiongozi wao" # Nyumba "nyumba" inawakilisha hekalu. # vipande sabini vya fedha Hii inamaanisha shekeli. Shekeli ina uzito wa gramu 11. "karibia kilo moja ya fedha" # Sabini "70" # Baali Berith Hili ni jina la mungu wa uongo. # wasio na sheria na wajinga "wakorofi na wajinga"