# Akatoka huko Hapa anazungumziwa Gideoni pamoja na askari waliomfuata. "Gideoni na watu 300 wakatoka huko" # Penieli Hili ni jina la mahali. # akawaambia watu maneno hayo hayo "akaomba chakula hapo kwa namna ile ile" au " pia akawaomba chakula" # Nitakapokuja kwa amani Hii ni namna ya heshima ya kuzungumza juu ya kumshinda adui. "Baada ya kumaliza kulishinda jeshi la Midiani" # nitauangusha mnara huu "Mimi" inawakilisha Gideoni na watu wake. "Watu wangu na mimi tutauangusha mnara huu"