# mama alichukua amri katika Israeli Hii inazungumzia juu ya uongozi wa Debora kama mama wa Israeli. "Aliwajali Waisraeli kama ambavyo mama anawajali watoto wake" # Walichagua miungu wapya "Wana wa Israeli waliabudu miungo mipya" # kulikuwa na vita katika malango ya jiji Neno "malango" linawakilisha mji mzima. "maadui waliwashambulia watu ndani ya miji ya Israeli" # hapakuwa na ngao au mikuki iliyoonekana kati ya watu elfu arobaini nchini Israeli. Hii sentensi inaelezea ni kwa kiasi gani Waisraeli walikuwa na silaha chache. # elfu arobaini nchini Israeli "40,000 nchini Israeli"