# Maelezo ya jumla Tazama; tafsiri ya majina # hawakuwaruhusu kuja bondeni "aliwakataza kushuka bondeni" # bonde eneo kubwa la ardhi lisilo na miti # Mlima wa Heresi Hili ni jina la mlima mkubwa ambapo mji wa Aiyaloni ulijengwa. # Aiyaloni... Shaalbimu, Haya ni majina ya miji # nguvu za kijeshi za nyumba ya Yusufu ziliwashinda "kabila la watu wa uzao wa Yusufu waliweza kuwashinda kwa sababu walikuwa na jeshi lenye nguvu" # Nyumba ya Yusufu Hapa "Nyumba" inamaanisha uzao. Manase na Efraimu walikuwa watoto wa Yusufu na "nyumba ya Yusufu" inaweza kuwa na maana ya uzao wa Manase na Efraimu. "uzao wa Manase na Efraimu" # kilima cha Akrabimu Hiki kilikuwa njiani kusini mashariki na Bahari ya shamu. Pia inaitwa "njia ya nge" # Sela Hili ni jina la mji