# jiji la Yerusalemu na kulichukua Hapa "jiji" lina maanisha watu. "watu wanaoishi Yerusalemu na kuwashinda" # Walishambulia Walishambulia jiji linaliwakilisha watu wa mji. "Walishambulia watu wa jiji" # kwa makali ya upanga Hapa "Upanga" inamaanisha upanga au silaha nyingine inayotumiwa na askari vitani. "na upanga wao" au "na silaha zao" # watu wa Yuda walikwenda chini kupigana Ilikuwa kawaida kutumia neno chini ikiwa ina maanisha kusafiri toka Yerusalemu. "Watu wa Yuda walikwenda kupigana" # Negebu Kusini mwa jangwa la Yuda # Milima vilima vilivyo chini ya mlima. # jina la Hebroni hapo awali ilikuwa Kiriath-arba Hii ni taarifa. baadhi ya watu ambao walisoma kitabu hiki mwanzoni yamkini walisikia juu ya Kiriath-arba lakini hawakufahamu kuwa ilikuwa ni mji wa Hebroni. # Sheshai, Ahimani na Talmai Haya ni majina ya viongozi watatu wa Kikanaani wa Hebroni. Kila kiongozi anawakilisha jeshi lake.