# Sentensi unganishi Yakobo anawatia moyo waamini waliotawanyika kuonyesha imani yao mbele za watu. Kama vile Abrahamu alivyoionesha imani yake kwa vitendo. # Kuna uzuri gani, ndugu zangu, kama mtu anasema ninayo imani, lakini hana matendo? Yakobo anatumia swali kuifundisha hadhira yake. "Waamini wenzanhu, sio vizuri kabisa mtu akisema ana imani lakini hana matendo." # anayo imani Yakobo anazungumzia imani, kumuamini Mungu. # haina matendo Yakobo anazungumzia matendo kuwa ni kufanya matendo mema. # Je, imani hiyo yaweza kumwokoa? Yakobo anazungumzia imani kuwa kumuamini Mungu kuna nguvu ya pekee katika kumuokoa mwanadamu lakini Imani haitoshi. "Imani hiyo haiwezi kumuokoa." # kumuokoa "Kumuokoa toka kwenye hukumu ya Mungu." # mkaote moto "kuwa na nguo za kutosha kuvaa" au "kuwa na sehemu ya kulala." # mle vizuri "kuwa na chakula cha kutosha." # ya mwili kula, kuvaa na kuishi vizuri. # yafaa nini? Yakobo anatumia swali hili kuifundisha hadhira. "hivi sio vizuri." # wa kiume na wa kike Waamini wenzangu katika Yesu, wanaume kwa wanawake # imani ... imekufa Yakobo anaizungumzia imani kuwa ni hai mtu afanyapo matendo mema na imekufa kama mtu hatafanya matendo mema. # imani ... ina matendo Imani inaambatana na mtu afanyaye matendo mema.