# Maelezo ya Jumla Yahwe anamaliza kuzungumza. # Watatoka nje Hapa "watatoka" ina maana ya watu wote, waaminifu wa Israeli na wageni, ambao huja kumwabudu Yahwe. # funza ... na moto Vishazi vyote viwili vinafafanua wazo moja kusisitiza adhabu ya Yahwe. # funza ambazo zinawala Funza zinawakilisha utisho wa kuoza ambao ni adhabu ya Yahwe kwa waovu. # moto unaoteketeza Moto pia unawakilisha hukumu ya Yahwe. # hautazimishwa Hii inaweza kuelezwa kwa chanya. "utachoma milele" # wote wenye mwili Msemo huu unawakilisha viumbe vyote hai vilivyoumbwa ambavyo hurudi kutoka kwa wafu.