# Maelezo ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza kwa wale wa Israeli ambao huabudu sanamu. # Tazama, watumishi wangu "Tambua na zingatia kwa makini" Yahwe anarudia hili kwa ajili msisitizo. # lakini utalia kwa sabubu ya maumivu ya moyo, na utaomboleza kwa sababu ya kupondwa kwa roho Vishazi hivi vina maana moja na marudio ni kwa ajili ya msisitizo. # kupondwa kwa roho Msemo huu unalinganisha hisia ya kuvunjwa moyo sana na majonzi kwa kitu kuharibika umbo kwa sababu ya shinikizo la juu.