# Taarifa ya Jumla Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza na Yahwe. # Miji yako mitakatifu imekuwa nyika Hii inasisitiza ya kwamba miji imeangamizwa na hakuna aishiye kule. # Hekalu letu takatifu na zuri, ambapo baba zetu walikusifu, limeangamizwa kwa moto Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Adui ameangamiza hekalu letu takatifu na zuri, pale ambapo baba zetu walikusifu, kwa moto" # Unawezaje kujizuia, Yahwe? Unawezaje kukaa kimya na kuendelea kutudhalilisha? Wanatumia maswali kuelezea kukata tamaa kwao kwa sababu Mungu bado hajaja kuwasaidia. "Tafadhali usijizuie, Yahwe! Tafadhali usikae kimya na kuendelea kutuaibisha!"