# Taarifa ya Jumla Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza na Yahwe. # na matendo yetu yote matakatifu ni kama kitambaa cha hedhi "Kitambaa cha hedhi" ni nguo ambayo mwanamke hutumia wakati wa mwezi anapotokwa damu kutoka kwenye tumbo la uzazi wake. Hii ina maana majaribio yao kumfurahisha Mungu yalishindikana. Sentensi hii ilikusudiwa kushtusha. # Tumenyauka wote kama majani Isaya analinganisha watu wa Israeli na majaniu ambayo hukauka yanapokufa. # Udhalimu wetu, kama upepo, unatubeba mbali Hii ina maana dhambi zao, kama jamii, ni sababu ya kushindwa kwao. Isaya analinganisha udhalimu na upepo kama nguvu ya mateso yao ya adhabu ya Yahwe. # umeficha uso wako kwetu Hii ina maana Mungu alikataa tamaa juu ya watu wake na kuwaacha wateseke.