# Taarifa ya Jumla Isaya anaendelea kuzungumza. # kuwapa ... kuwapatia Isaya anarudia hivi kusisitiza. # kilemba "kilemba cha kichwani" au "kifuniko kizuri cha kinywani". Hii ni kitambaa kirefu cha nguo kinachozunguka kichwa. # mafuta ya furaha ... joho la sifa Watu huweka mafuta juu yao na kuvaa joho zuri, ndefu wakati wa sherehe na shangwe. # katika nafasi ya roho ya kutojali "katika nafasi ya huzuni" au "katika nafasi ya maombolezo" # mwaloni wa utakatifu, kupandwa kwa Yahwe Hii ina maana Yahwe amesababisha watu kuwa na nguvu na imara. # ili aweze kutukuzwa Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ili kwamba maisha ya watu yaweze kumtukuza yeye"