# Maelezo ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli. # kwa maana Yahwe atakuwa nuru yako ya mlele Mistari miwili inarudia wazo hili moja kwa msisitizo. # Jua lako halitazama tena, wala mwezi wako hautaondoka na kupotea Mwezi hautapotelea kihalisia. Hii ni kusema ya kwamba kulinganisha na mwanga wa Yahwe, mwanga wa jua na mwezi hautakuwa kitu.