# Maelezo ya Jumla Isaya anaendelea kzungumza na watu wa Israeli. # Miguu yao hukimbilia uovu "Miguu" inawakilisha uwezo wa kuondoka na "kukimbia" ina maana ya kufanya jambo kwa haraka. "Wana haraka ya kufanya mambo maovu" # ni njia zao "njia" inawakilisha njia yao ya maisha. "ni yote wanayofanya" # hakuna haki katika njia zao "njia" inawakilisha njia yao ya maisha. "kamwe hawafanyi kilicho haki" au "kila kitu wafanyacho sio cha haki" # Wametengeneza njia zilizopinda "Njia zilizopinda" inawakilisha njia ya maisha ambayo imepotoka. "Wanasema na kufanya mambo yasiyo ya kweli. Ni wajanjawajanja"