# Maelezo ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza. # njia zake "njia zao". Hapa "zake" ina maana ya watu wa Israeli. # fariji na tuliza wale ambao wanaomboleza kwa ajili yake "Nitabembeleza na kutuliza wale ambao wanahisi huzuni kwa ajili ya mateso ya watu kwa sababu ya tabia yao ya dhambi" # na ninatengeneza matunda ya midomo Hapa "matunda ya midomo" ina maana ya kile mtu anachosema. "na ninasababisha wao wanisifu na kunishukuru" # Amani, amani, kwa wale ambao wapo mbali sana "Nimefanya amani pamoja nao ambao wako mbali" Neno "Amani" linarudiwa kwa msisitizo.