# Mtafute Yahwe wakati bado anaweza kupatikana Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mtafute Yahwe wakati bado unaweza kumpata" # Na muovu aache njia yake Neno "muovu" una maana ya watu waovu. Yahwe anazungumzia watu waovu kutofanya dhambi tena kana kwamba walikuwa wakiacha kutembea katika njia ambayo walikuwa wakisafiria. "Na watu waovu wabadili namna wanavyoishi" # na mwanamume wa dhambi mawazo yake Kitenzi unaweza kutumika kutoka katika msemo uliopita. "na mwanamume mwenye dhambi aache mawazo yake" # mawazo yake Maana zaweza kuwa 1) "namna anavyofikiri" au 2) "mipango yake" # naye atamhurumia "na Yahwe atamhurumia" # na kwa Mungu wetu Kitenzi kinaweza kutumika kutoka kwa msemo wa kwanza katika sentensi hii. "na mruhusu arudi kwa Mungu wetu"