# Maelezo ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli. # Mimi, mimi, ndiye yeye Neno "Mimi" inarudiwa kwa msisitizo. # Kwa nini unawaogopa wanadamu ... kama nyasi? Swali hili la balagha linasisitiza ya kwamba watu ambao wana ulinzi wa Mungu wanatakiwa kutowaogopa wanadamu. Hii inaweza kuandikwa kama kauli. "Usiogope wanadamu ... kama nyasi" # ambao wametengezwa kama nyasi Msemo huu unalinganisha wanamume na nyasi kusisitiza ya kwamba maisha yao ni mafupi na kwamba wanakufa upesi. "ambao wanaishi na kufa haraka kama nyasi" au "ambao watanyauka na kutoweka kama nyasi" # ambao wametengezwa kama Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambao ni kama"