# Maelezo ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli. # Inua macho yako mbinguni Kuinua macho inawakilisha kutazama kitu kilicho juu. "Tazama juu angani" # kama moshi ... kama vazi ... kama nzi Zote hizi zina maana ya vitu ambavyo hutoweka kwa haraka na kirahisi au kutokuwa na thamani. # wokovu wangu utaendelea milele "wokovu" wa Mungu hapa unawakilisha matokeo ya wokovu wake, ambayo ni uhuru. "Nitakuokoa, utakuwa huru milele" # haki yangu haitakoma kutumika "haki" ya Mungu hapa inawakilisha yeye kutawala kwa haki. "utawala wangu wa haki hautakuwa na mwisho" au "nitatawala kwa haki milele"