# Taarifa ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza na Sayuni kana kwamba ilikuwa mwanamke. # Je! mali iliyoibiwa inaweza kuchukuliwa kutoka kwa hodari, au mateka kuokolewa kutoka kwa jeshi kali? Isaya anatumia swali kuelezea ugumu wa kuchukua kitu chochote kutoka kwa mwanajeshi mwenye uwezo au hodari mwenye nguvu sana. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mtu hawezi kuchukua mali iliyoibiwa kutoka kwa hodari au kuokoa mateka kutoka kwa wanajeshi wakali" # mali iliyoibiwa vitu vya thamani vilivyochukuliwa kutoka kwa walioshindwa katika vita. # mateka watachukuliiwa mbali kutoka kwa hodari, na mali iliyoibiwa itaokolewa Yahwe anasema ya kwamba atafanya kile ambacho kawaida hakiwezekani kwa watu kufanya. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Nitachukua mateka kutoka kwa hodari, na nitaokoa mali iliyoibiwa" # Nita ... kuokoa watoto wako Yahwe anazungumzia watu ambao wataishi Sayuni kana kwamba walikuwa watoto wa mji.