# Sikia haya "Sikiliza ujumbe wangu". Yahwe anazungumza. # nyumba ya Yakobo Hapa "nyumba" ina maana ya vizazi vya Yakobo. "vizazi vya Yakobo" # ambao wameitwa kwa jina la Israeli Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambao kila mtu huwaita watu wa Israeli" # wametokana na mbegu ya Yuda Msemo huu unasisitiza ya kwamba ni vizazi vya moja kwa moja, vya kimwili vya Yuda. "ni vizazi vya Yuda" # kumsihi Mungu wa Israeli "kumwita Mungu wa Israeli" # wanajiita wenyewe Hii ina maana ya wtu wa Israeli. "mnajiita wenyewe" # mji mtakatifu Hii ina maana ya Yerusalemu. # Yahwe wa majeshi Yahwe wa majeshi ya Israeli