# Taarifa ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza na Kosheri. # na kusawazisha milima Yahwe anazungumza kuondoa vizuizi ambavyo vinaweza kukawiza mafanikio ya Koreshi kana kwamba ilikuwa kusawazisha milima mbele yake. # milima Neno la Kiebrania linalotumika katika maandishi ni adimu na maana haileweki. Baadhi ya tafsiri zina "sehemu za kukwaruzakwaruza" au "sehemu zilizopinda". # nguzo zao za chuma Hii ina maana ya nguzo za chuma katika malango ya shaba. # hazina za giza Hapa "giza" ina maana ya sehemu ambazo ni za siri. "hazina katika sehemu za giza" au "hazina katika sehemu za siri"