# Taarifa ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza # Yakobo, na Israeli Hii ina maana ya watu waliotokana kwa Yakobo, Israeli. "nyie uzao wa Israeli" # hautasahaulika na mimi Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Sitakusahau" # Nimefuta, kama wingu zito, matendo yako ya uasi, na kama wingu, dhambi zako Kauli hizi mbili zina maana ya kitu kimoja. Mungu ameondoa dhambi zao kwa haraka na urahisi kama upepo uweze kupuliza mbali wingu. # na kama wingu, dhambi zako Kitenzi kinaweza kutumika kutoka na msemo uliopita. "na kama wingu, nimefuta dhambi zako"