# Taarifa ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli. # nitasema kwa kaskazini ... kwa kusini Yahwe anazungumza kwa "kaskazini" na "kwa kusini" kana kwamba anaamuru mataifa katka maeneo hayo. # wana wangu ... binti zangu Yahwe anazungumzia wtu ambao wanakuwa wake kana kwamba walikuwa watoto wake. # kila mtu ambaye ameitwa kwa jina langu Hapa kuitwa kwa jina la mtu inawakilisha kuwa mali ya mtu huyo. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kila mtu ambaye nimemuita kwa jina langu" au "kila mtu ambaye ni mali yangu" # ambaye nimemuumba, ndio, ambaye nimemtengeneza Zote hizi zina maana moja na husisitiza ya kwamba ni Mungu ambaye aliwatengeneza watu wa Israeli.