# Taarifa ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza # wewe kiziwi ... wewe kipofu Hapa "wewe" ni wingi na ina maana ya watu wa Israeli. Yahwe anazungumzia kushindwa kwao kumsikliza na kumtii kana kwamba walikuwa viziwi na vipofu. # Ni nani aliye kipofu ila mtumishi wangu? Au kiziwi kama mjumbe wangu nayemtuma? Yahwe anauliza maswali haya ya balagha kukaripia watu wake na kusisitiza ya kwamba hakuna mtu aliye kipofu au kiziwi kama walivyo. "Hakuna mtu aliye kipofu kama mtumishi wangu. Hakuna mtu aliye kiziwi kama mjumbe wangu ambaye namtuma" # Ni nani aliye kipofu kama mwenzangu wa agano, au kipofu kama mtumishi wa Yahwe? Yahwe anauliza maswali haya ya balagha kukaripia watu wake na kusisitiza ya kwamba hakuna mtu aliye kipofu au kiziwi kama walivyo. "Hakuna aliye kipofu kama mwenzangu wa agano. Hakuna aliye kipofu kama mtumishi wa Yahwe".