# Taarifa ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza. # Waache watoe utukufu Hapa "waache" ina maana ya watu katika nchi za pwani. # Yahwe atatoka nje kama hodari; kama mwanamume wa vita Yahwe analinganishwa na hodari ambaye yupo tayari kuwashinda watu wa adui zake. # atamwamsha ari yake Hapa "ari" ina maana ya uchu ambao hodari hupitia anapokaribia kupigana vita. Yahwe kuchangamsha ari yake inazungumziwa kana kwamba aliamsha kama upepo unapoamsha mawimbi ya maji.