# Tazama ... angalia Maneno haya huongeza msisitizo kwa kile kinachofuata. # mataifa ni kama tone katika ndoo, na yanachukuliwa kama vumbi katika mizani Nabii analinganisha mataifa kwa tone la maji na kwa vumbi ili kusisitiza jinsi yalivyo madogo na kutokuwa na umuhimu kwa Yahwe. # kama tone katika ndoo Maana zaweza kuwa 1) tone la maji ambalo huanguka katika ndoo au 2) tone la maji ambalo hudondok nje ya ndoo. # na wanachukuliwa kama vumbi katika mizani Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "na Yahwe anawachukulia kama vumbi juu ya mizani" # yanachukuliwa na yeye kama si kitu Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "anayachukulia kutokuwa kitu"