# Maelezo ya Jumla Hezekia anaendelea maombi yake ya maandishi. # Kama mbayuwayu ninalia; ninalia polepole kama njiwa Vishazi hivi vyote viwili vina maana moja na vinasisitiza jinsi milio ya huzuni na kusikitisha ya Hezekia ilivyokuwa. Mbayuwayu na njiwa ni aina ya ndege. "Milio yangu ni ya kusikitisha - inasikika kama mlio wa mbayuwayu na sauti kama ya njiwa" # macho yangu Hapa Hezekia ana maana ya yeye mwenyewe. "macho" yake yanasisitiza ya kwamba anatafuta kitu. # kwa kutazama juu Hii ina maana ya Hezekia kutazama mbinguni kwa ajili ya Mungu kumsaidia. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "kwa kusubiri msaada unaokuja kutoka mbinguni" au "kwa kusubiri kwa ajili yako kunisaidia" # Ninaonewa Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ugonjwa wangu unanitesa mimi" # Niseme nini? Hezekia anatumia swali kusisitiza hana chochote cha kusema. "Sina chochote kilichobaki cha kusema" # Nitatembea polepole Hii ni lahaja. Hapa "kutembea" ina maana ya kuishi. "Nitatembea kwa unyenyekevu" # miaka yangu yote Hii ina maana ya maisha yake yote yaliyobaka. "maisha yangu yaliyobaki" # kwa sababu nimezidiwa na majonzi "kwa sababu nimejaa majonzi" au "kwa sababu nina huzuni sana"