# Taarifa ya Jumla Hezekia anaendelea kuomba kwa Yahwe. # ambaye alimtuma Hezekia anamaanisha barua kutoka kwa Senakeribu. Maana ya hii inaweza kuwekwa wazi. "katika ujumbe aliotuma" # Geuza sikio lako "Tega sikio lako" au "Geuza kichwa chako". Hii ina maana kugeuza kichwa chako ili kwamba uweze kusikia jambo vizuri. # Senakeribu Hili ni jina la mfalme wa Ashuru. # mataifa yote na nchi zao Huku ni kukuza. Wafalme walikuwa wameangamiza nchi nyingi za karibu, lakini sio nchi zote. "mataifa mengi na nchi zao"