# Lakishi Huu ni mji kusini magharibi mwa Yerusalemu. # Senakeribu Hili ni jina la mfalme wa Ashuru. # Libna Huu ni mji kusini mwa Yuda. # Tirhaka mfalme wa Ethiopia na Misri wamehasamisha kupigana dhidi yao "Tirhaka" ni jina la mwanamume. Aliwahamasisha jeshi lake ili wawe tayari kupigana. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Tirhaka mfalme wa Ethiopia na Misri alihamasisha jeshi lake" # kupigana dhidi yake Neno "yake" inawakilisha Senakeribu. Msemo huu una maana ya kupigana dhidi ya jeshi la Senakeribu" # Yerusalemu haitatolewa katika mkono wa mfalme wa Ashuru Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Neno "mkono" lina maana ya nguvu ya kijeshi ya mfalme. "Mfalme wa Ashuru na jeshi lake halitakushinda katika Yerusalemu"