# Kamba zako ni goigoi; haziwezi kushikilia mlingoti mkuu katika sehemu yake; hawawezi kulitandaza tanga Maana zaweza kuwa 1) jeshi la Ashuru ni kama mtumbwi ambao hauwezi kusogea katikati ya maji: kamba ambazo hushikilia mlingoti mkuu na tanga zimekuwa legevu na hazishiki tena mlingoti mkuu, kwa hiyo tanga halina faida (33:1) au 2) watu wa Yuda hawapo vitani tena. "Umelegeza kamba ambazo zilishikilia nguzo zako za bender; bendera haipepei tena" # mlingoti mkuu nguzo ndefu ambazo hushikilia tanga # tanga kitambaa kikubwa ambacho hujazwa na upepo na kusogeza mtumbwi katikati ya maji # mali kubwa iliyoibiiwa itakapogawanywa Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watakapogawanya hazina" # vilema Hii ina maana ya watu ambao hawawezi kutembea. "wale ambao ni vilema" # watu wanaoishi pale watasamehewa kwa udhalimu wao Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atasamehe dhambi za watu wanaoishi pale"