# Nchi inaomboleza na kunyauka Hii inazungumzia nchi kuwa kavu kana kwamba ilikuwa mtu anayeomboleza. "Nchi kuwa kavu na mimea yake kunyauka" # anaona aibu na ananyauka Hii inazungumzia miti ya Lebanoni kunyauka na kuoza kana kwamba Lebanoni ilikuwa mtu ambaye ameaibika. "Miti ya Lebanoni hunyauka na kuoza" # Sharoni ... Bashani ... Karmeli Miti mingi na maua iliwahi kuota katika maeneo haya. # Sharoni ni kama jangwa wazi Hii inalinganisha jinsi Sharoni ilivyo kavu kwa jangwa wazi. "Sharoni ni kavu kama jangwa wazi" # Bashani na Karmeli hutikisa majani yao "hakuna majani tena katika miti ya Bashani na Karmeli"