# Taarifa ya Jumla Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda. # Atatoa "Yahwe atatoa" # mkate kwa wingi kutoka ardhini Hapa "mkate" unawakilisha chakula kwa ujumla. "atasababisha ardhi kutoa chakula kingi kwa ajili yako kula" # Katika siku hiyo Hapa "siku" inawakilisha kipindi cha muda kwa ujumla. "Katika kipindi hicho" # ambayo imepepetwa kwa koleo na uma Makoleo na uma yalitumika kurusha nafaka angani ili upepo upulize makapi, kuacha tu sehemu ambayo inaweza kuliwa. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambayo umepepeta kwa koleo na uma ya nyasi"