# Taarifa ya Jumla Isaya anafafanua jinsi Yahwe ataangamiza watu wa Yuda. # Ativunja Hapa "ataivunja" ina maana ya sehemu ya ukuta ambayo inakaribia kuanguka. Sehemu katika ukuta ni sitiari ambayo inawakilisha watu wa Yuda na dhambi yao iliyotajwa katika 30:12 # kama chombo cha mfinyanzi kinavyovunjwa Tashbihi hii ina maana ya kwamba kipande cha ukuta kitavunjika haraka na kikamilifu kama jagi la udongo linapoanguka chini. # mfinyanzi Mfinyanzi ni mtu ambaye hutengeneza vyungu na majagi kwa udongo. # hakutapatikana Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "hakuna mtu ataweza kupata" au "hapatakuwa" # kigae ambacho kitatumika kukwangua "kigae kikubwa ya kutosha kukwangua" # moto kutoka katika meko Neno "moto" hapa lina maana ya majivu. "majivu kutoka katika sehemu ya moto"