# Taarifa ya Jumla Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Yuda. # Kwa hiyo ulinzi wa Farao utakuwa aibu yako, na kimbilio katika kivuli cha Misri, fedheha yako Hii inaweza kuandikwa ili kwamba nomino dhahania "ulinzi", "aibu", na "fedheha" zinaelezwa kama vivumishi au vitenzi. "Kwa hiiyo utaibika kwa sabbu ulimtegemea Farao kukulinda; utafedheheshwa kwa sababu uliwategemea Wamisri kukuweka salama" # kimbilio katika kivuli cha Misri Ulinzi wa Misri kutoka kwa jeshi la adui inazungumziwa kana kwamba ulikuwa kivuli ambacho humlinda mtu kutoka na joto linalowaka la jua. # wakuu Hapa "wakuu" ina maana ya afisa au balozi, sio lazima wana wa mfalme. # wao ... wata ... wao Maneno haya yana maana ya watu wa Yuda. # Soani ... Hanesi Hii ilikuwa miji katika sehemu ya kaskazini ya Misri. # wamekuja Hanesi Hapa "kuja" inaweza kuandikwa kama "kuondoka" # kwa sababu ya watu "kwa sababu ya watu wa Misri"