# Kauli Kiunganishi Hii inaendelea kuzungumza kuhusu watu wa Israeli kana kwamba walikuwa shamba la mizabibu. # Sina hasira, Oh, hata kuwe na mibigili na miiba! Katika vita nitatembea dhidi yao "Sina hasira. Kama kulikuwa na mibigili na miiba ningetembea dhidi yao katika vita" # Sina hasira Inaeleweka ya kwamba Yahwe hana hasira na watu wake tena. "Sina hasira na watu wangu tena" # hata kuwe na mibigili na miiba Adui za watu wa Israeli wanazungumziwa kana kwamba walikuwa mibigili na miiba inayoota katika shamba la mizabibu. # mibigili na miiba Mibigili na miiba hutumika mara kwa mara kama alama ya miji na nchi zilizoharibiwa # Katika vita nitatembea dhidi yao Yahwe kupigana na adui zake inazungumziwa kana kwamba alikuwa mwanajeshi katika jeshi. # Ningetembea dhidi yao; Ningewachoma wote kwa pamoja Hapa Isaya anaunganisha picha tofauti kuzungumzia maadui wa Yahwe. Anazungumza juu yao kana kwamba walikuwa mibigili na miiba lakini pia kama wanajeshi katika jeshi. # isipokuwa washike ulinzi wangu Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "ulinzi" ielezwe kama kitenzi "kulinda". "Isipokuwa waniulize kuwalinda wao" # na kufanya amani pamoja na mimi; waache wafanya amani pamoja na mimi "na waombe kuishi kwa amani pamoja nami; ninataka waishi kwa amani pamoja nami"