# mkono wako umeinuliwa juu Yahwe kujiandaa kuwaadhibu watu waovu inazungumziwa kana kwamba mkono wake uliinuliwa na unataka kuwapiga watu waovu. # lakini hawagundui "lakini watu waovu hawagundui" # wataona ari yako kwa ajili ya watu Hapa "kuona" inawakilisha kugundua kitu. "watagundua ya kwamba una hamu ya kuwabariki watu wako" # kuaibishwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "wataaibishwa" # moto wa adui zako utawaangamiza Yahwe kuwaadhibu na kuwaangamiza kabisa adui zake inazungumziwa kana kwamba angetuma moto ambao utawachoma kabisa. # moto wa adui zako Hapa "wa" haimaanishi moto ni wa maadui lakini ya kwamba moto umekusudiwa kutumiwa dhidi ya maadui. "moto wako utawachoma kabisa" # kwa ajili yetu Hapa "yetu" ina maana ya Isaya na inajumlisha watu wote wenye haki.