# Katika siku hiyo Hapa "siku" inawakilisha kipindi cha muda kwa ujumla. "Katika kipindi hicho" # wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "watu katika nchi ya Yuda wataimba wimbo huu" # Tuna mji imara Hii ina maana ya mji wa Yerusalemu. # Mungu amefanya wokovu ukuta na boma lake Nguvu ya Mungu kuwalinda na kuwaokoa watu wake inazungumziwa kana kwamba wokovu wake ulikwa ukuta unaozunguka mji. # taifa lenye haki linaloshikilia imani Hapa "taifa" inawakilisha watu. "watu wenye haki na waaminifu"