# Katika mlima huu Hii ina maana ya Yerusalemu au Mlima Sayuni. # Yahwe wa majeshi Yahwe wa majeshi ya Israeli. # karamu ya vitu vinono Hapa "vitu vinono" ina maana ya vyakula bora. # karamu katika masimbi "divai ya zamani". Hii ina maana ya divai bora. # kifuniko juu ya watu wote, utando ulifumwa juu ya mataifa Kifo, mateso, na huzuni inazungumziwa kana kwamba vilikuwa wingu jeusi au utando ambao hufunika kila mtu juu ya dunia. # Ataimeza mauti milele Yahwe kusababisha watu kuishi milele inazungumziwa kana kwamba angeweza kumeza kifo. # aibu ya watu wake ataiondoa kutoka dunia nzima Yahwe kusababisha watu kutokuwa na aibu tena inazungumziwa kana kwamba aibu ilikuwa kitu ambacho Yahwe angeweza kuondoa mbali.