# Itakuja kuwa Hii inaweka alama kwa tukio muhimu. # katika siku hiyo Hapa "siku" ina maana ya kipindi cha muda kwa ujumla. "katika kipindi hicho" # wingi wa walio juu Msemo "wingi" au "jeshi" ni neno ambalo lina maana ya idadi kubwa ya kitu. Hapa ina maana ya viumbe viovu vya kiroho katika mbingu. "viumbe viovu vya kiroho" au "malaika ambao waliasi dhidi yake" # walio juu Hapa "juu" inawakilisha mbinguni au anga. "katika mbingu" au "katika anga" # Watakusanywa pamoja, wafungwa katika shimo, na watafungwa katika gereza Hapa "shimo" ina maana ya chumba chenye giza au shimo katika gereza. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawakusanya pamoja kama wafungwa wake na kuwafunga katika gereza la chini" # wataadhibiwa Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe atawaadhibu" # Kisha mwezi utaaibishwa, na jua kufedheheshwa Jua na mwezi inaelezwa kama mtu ambaye anaona aibu ya kuwa mbele ya mtu mwenye nguvu kubwa. Katika uwepo wa Yahwe, nuru ya mwezi na jua itaonekana na mwanga mdogo.