# Shebna Hili ni jina la msimamizi wa kasri ya mfalme huko Yerusalemu. # ambaye yupo juu ya nyumba Hapa "nyumba" inawakilisha wale walio katika kasri ya mfalme. "ni nani aliye msimamizi wa wale ambao wanafanya kazi katika kasri" # Unafanya nini hapa na nani amekupa ruhusa ... katika mwamba? Yahwe anatumia swalii hili kumkaripia Shebna. "Hauna haki ... katika mwamba!" # kukata kaburi ... kuchonga kaburi ... kuchonga sehemu ya kupumzika Misemo hii mitatu yote ina maana ya kutengeneza kaburi la kuzika. # juu ya marefu Watu muhimu zaidi wa Israel walikuwa na makaburi katika sehemu za juu.