# Tamko "Hivi ndivyo Yahwe anavyotamka" au "Huu ni ujumbe kutoka kwa Yahwe" # kuhusu Duma Hili ni jina lingine kwa ajili ya Edomu. Hapa "Duma" inawakilisha watu wanaoishi kule. "kuhusu watu wa Duma" au "kuhusu watu wa Edomu" # Mtu ananiita kwangu Hapa "ananiita" ina maana ya Isaya. # Seiri Hili ni jina la milima ya magharibi mwa Edomu. # Mlinzi, nini kimebaki usiku? Mlinzi, nini kimebaki usiku? Hii inarudiwa kusisitiza ya kwamba mtu yule anayeuliza swali ana wasiwasi na woga. # kama unataka kuuliza, basi uliza; na urudi tena "Niulize sasa kile unachotaka kujua, lakini pia uje baadaye uniulize tena"